Britony Jonas

KIPIMO CHA UPENDO

UTAJUAJE KUWA UNA UPENDO? JIBU NI  MARKO 12:28-31.

Upendo hudhihirishwa kupitia mahusiano ya aina mbili tu:
1. Kumpendeza Mungu kwa: 1.Moyo wote; 2. Roho yote; 3. Akili yote; na 4. Nguvu zote. Upendo kwa Mungu hudhihirishwa na KUJITOA KWAKE, (Total Surrender), bila kubakiza kitu.

Wengi  wetu huonyesha kumpenda kwa kutoa baadhi ya vitu tu lakini sio vyote. Kutoa mwili wote ili uwe makao  ya Roho Mtakatifu,  limekuwa jaribu gumu kwa wengi wetu. Utekelezaji wa kauli ya Warumi 12:1,2, tumeshindwa wengi na tumetekwa na mwendo wa dunia, kimwonekano na kivipaumbele. Hivyo Zaka na sadaka hutumiwa nasi kama kumkopa Mungu ili turudishwe baadaye, kisha milango ya kupata tena kujifunga na kujikuta tunaishi kama wadeni,  wasio na mibaraka.

2. Kumpenda Jirani/ mwenzako kama nafsi yako.
Jirani wa kwanza hutakiwa kuwa ni mwanafamilia, mzazi au mtoto, kwa mujibu wa 1 Timotheo 5:1-8; Waef 6:1-4; Kutoka 12:12.

Kuonyesha UPENDO - kwa watu wa nyumbani mwetu ndiyo ajenda ya kwanza. Kumbuka hawa watu wa nyumbani ndio tunaosumbuana zaidi, maana maisha ya Uadui huonyeshwa zaidi miongoni mwao. Kupitia hawa wanafamilia tumepewa Kujifunza kupenda  na kupendana,  tukitumia: MOYO WA REHEMA; UTU WEMA; UPOLE; UVUMILIVU;WEMA; UNYENYEKEVU; KIASI, AMANI,IMANI;  na Matunda mengine yaliyoorodheshwa na Mtume Paulo katika Wakolosai 3:12; Wagalatia 5:22,23; Waef 4:2;Waeb 11:1,  na Petro katika 2Petr 1:3-11.

Kanisani ni rahisi Kuishi kiprogramu kwa Kujifunza jinsi ya kusema na jinsi ya kuitikia kisalamu. Tunalazimishana haya kila mara mpaka tucheke wakati sio muda wake, au kusema amina wakati ulimi ni mzito kuamka.

HABARI NJEMA KUHUSU NYUMBANI

1. Maisha nyumbani  ni HALISI. Sio rahisi kulazimishana kufurahi au kukasirika, au kupenda.

2. Maisha ya nyumbani sio rahisi kuyaigiza. Maneno husikika ambayo hukujiandaa jinsi ya kuyasema na kuyajibu na yanataka majibu pengine ya haraka.  Matendo hutokea yasiyotarajiwa wakati mwingine.

 Siyo rahisi Kuishi kiprogramu nyumbani kama itokeavyo  kanisani, maana sahani na vikombe/glasi nyumbani havivunjiki kiprogramu. Aidha kuku/mifugo inapoachiwa hujilisha bila programu.

 Aidha maneno ya kukabiliana na hizo hasara nayo hayaandaliwi mdomoni. Matokeo  yake huwa ni kukosa UVUMILIVU,  UPOLE, MOYO WA REHEMA, KIASI, na hivyo kutumia kauli za kimamlaka. " Nimesema kama...Nione tena mtu akifanya hili... Nisisikie tena hizo kelele zenu na...

Kwa kuogopa mamlaka nyumba hupata UKIMYA lakini siyo UTULIVU wala AMANI, maana wanafamilia  wamejawa na Hofu na woga. Mambo yao sasa hufanyia sirini, ambako, hata mwenye mamlaka hana mamlaka nako maana hapajui ni wapi. Wazazi wengi tuna mamlaka nyumbani kimwonekano, lakini hatuna mamlaka katika siri za watoto wetu. Hii ndiyo sababu Hutuaibisha kwa KUPATA MIMBA au KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA. N.k

Mazingira aina hii ndiyo yanatawala Kaya na Familia nyingi. Inabidi kila mwenye kuielewa kuwa ni mwenye mamlaka nyumbani, ajue mpaka yake na kuomba Mungu ajuaje sirini amsaidie KUIPATANISHA Familia yake, akitumia ujumbe wa Eliza Nabii, (Malaki 4:5,6 ), kwa kuwezesha na Matunda ya Roho yanayoelezwa ndani ya Makesha ya Machi 6-15+. Kama haya yamekusaidia kuleta matengenezo ya kiroho ndani ya familia yako tuma kwa familia 5 zingine. Mimi nimechagua familia yako. Barikiwa unapofanya jukumu hili. 
Britonyjonas@gmail.com @2018

Comments

Popular posts from this blog