Mungu akiwa upande wetu nani wa kutusumbua? Katika utulivu wake katika mji wa Arusha nikitafakari ukuu wa Mungu aliye hai.
Britonyjonas MUNGU NDIYE MWEMA. JE, YESU NI MWEMA? Leo nitajibu HOJA ya salam ya Mungu Ndiye Mwema. Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidni wamekuwa na tabia ya kutumia aya 18-19 iliyopo katika Luka Sura ya 18, inayo sema Mungu Ndiye Mwema. Waislam wanadai kuwa, katika aya hii, Yesu amekana kuwa yeye si "MWEMA" na kuwa Mungu Pekee ni Mwema, hivyobasi, kukana kwa Yesu kuwa yeye si Mwema kunapinga Madai ya Wakristo kuwa Yesu ni Mungu. Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema kuwa eti Yesu amekana kuwa yeye si MWEMA. Fundisho hili la "MUNGU PEKEE NDIYE MWEMA" wanalieneza kwa kupitia Mitandao mbalimbali kama ya Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingaw...
Comments
Post a Comment