Wimbo huu huwa unanibariki sana hata pale mambo yanapokuwa magumu Munguvhusimama ndipo napata nafasi ya kusifu zaidi jina lake maana anajibu kwa wakati. 3 - Mungu Atukuzwe. 1 Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu, Upendo wake ulitupa Yesu, Aliyejitoa maisha yake, Tuwe nao uzima wa milele. CHORUS: Msifu, msifu, dunia sikia, Msifu, msifu watu wafurahi, Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana, Ukamtukuze kwa mambo yote. 2 Wokovu kamili, zawadi kwetu, Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu, Wanaomwamini na kuungama, Mara moja wale husamehewa. 3 Alitufundisha mambo makuu, Alihakikisha wokovu wetu, Lakini zaidi ajabu kubwa, Yesu atakuja na tutamwona.