Britony Jonas KIPIMO CHA UPENDO UTAJUAJE KUWA UNA UPENDO? JIBU NI MARKO 12:28-31. Upendo hudhihirishwa kupitia mahusiano ya aina mbili tu: 1. Kumpendeza Mungu kwa: 1.Moyo wote; 2. Roho yote; 3. Akili yote; na 4. Nguvu zote. Upendo kwa Mungu hudhihirishwa na KUJITOA KWAKE, (Total Surrender), bila kubakiza kitu. Wengi wetu huonyesha kumpenda kwa kutoa baadhi ya vitu tu lakini sio vyote. Kutoa mwili wote ili uwe makao ya Roho Mtakatifu, limekuwa jaribu gumu kwa wengi wetu. Utekelezaji wa kauli ya Warumi 12:1,2, tumeshindwa wengi na tumetekwa na mwendo wa dunia, kimwonekano na kivipaumbele. Hivyo Zaka na sadaka hutumiwa nasi kama kumkopa Mungu ili turudishwe baadaye, kisha milango ya kupata tena kujifunga na kujikuta tunaishi kama wadeni, wasio na mibaraka. 2. Kumpenda Jirani/ mwenzako kama nafsi yako. Jirani wa kwanza hutakiwa kuwa ni mwanafamilia, mzazi au mtoto, kwa muj...